Wednesday, 17 February 2016

JINSI YA KUPIKA MAANDAZI, FATA HATUA HIZI

JINSI YA KUPIKA MAANDAZI.
Vipimo

Unga 5 Vikombe

Tui la Nazi zito vugu vugu 1 ¼ kikombe

Sukari 3/4 kikombe cha chai

Samli iliyoyayushwa au mafuta 3 vijiko vya Supu

Hamirah 2 Vijiko vya Supu

Hiliki 1/2 Kijiko cha chai

Mafuta ya kukaangia

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

1. Ndani ya kibakuli kidogo, mimina hamira na na vijiko viwili vya kulia vya tui. Weka kando mpaka hamira ianze kufura, kama dakika 5-10.

2. Pasha samli moto

3. Ndani ya bakuli kubwa au sinia, changanya unga, sukari, iliki na samli ikiwa bado moto moto.

4. Mimina hamira ndani ya mchanganyiko wa unga. Changanya na ukande huku ukitumia lile tui la nazi. Tui likipungua unaweza ukaongeza maziwa. Kanda unga mpaka uwe laini.

5. Kata madonge *12 au 15 uyaweke kwenye baraza iliyonyunyiziwa unga na uyafunike ili yapate kufura na yasikauke. *Ukipenda maandazi manene fanya madonge 12. Ukipenda mepesi fanya madonge 15
7. Pasha mafuta moto kwenye karai. Maandazi yako tayari kukaangwa sasa.

8. Kaanga maandazi kwenye mafuta ya moto. Upande mmoja ukifura na kuwa rangi nzuri geuza upande wa pili. Endelea nama hii mpaka maandazi yote yawe tayari.

No comments:

Post a Comment